KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 1, 2011

Steven Pienaar AWATAKA BAFANA BAFANA KUJITUMA MBELE YA MISRI.


Kiungo wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza Steven Pienaar amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya Afrika kusini kuwa makini na mchezo ujao wa kuwani nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2012 utakao wakutanisha na mabingwa watetezi Misri.

Steven Pienaar ametoa rai hiyo kwa wachezaji wenzake, huku akidai kwamba endapo watashindwa kuutilia maanani mchezo huo kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza malengo ya kufanya vyema kama mikakati ilivyopangwa huko nchini kwao Afrika kusini.

Amesema kila mmoja wao hana budi kujikubali yeye mwenyewe kwanza, na kisha kujitengenezea mazingira ya kujiandaa kimwili na kiakili kuwakabili mafarao ambao kwa sasa wanaburuza mkia wa kundi saba ambalo linaongozwa na timu ya taifa ya Afrika kusini.

Pienaar amesema endapo watapata matokeo ya sare katika mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa juma lijalo atafurahishwa na hatua hiyo lakini atasikitishwa sana endapo watakubali kufungwa.

Endapo timu ya Afrika kusini itafanikiwa kushinda katika mchezo huo itakata tiketi ya kufuzu fainali za mataifa ya bara la Afrika za mwaka ujao zitakazifanyika nchini Gabon and Equatorial Guinea kwani timu hiyo itafikisha point 10.

No comments:

Post a Comment