KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, June 13, 2011

TP MAZEMBE KUBISHA HODI FIFA.


Mabingwa wa soka barani Afrika Tp Mazembe, wamebadili mpango wao wa kukata rufaa katika mahakama a ya upataishi ya michezo CAS na badala yake wanajipanga kuwasilisha rufaa hiyo kwenye ofisi za shirikisho la soka ulimwenguni FIFA zilizopo huko mjini Zurich nchini Uswiz.

TP Mazembe wanatarajia kuwasili rufaa hiyo ya kupinga maamuzi ya shirikisho la soka barani Afrika CAF ya kuwaondoa kwenye michuano ya klabu bingwa barani humo katika msimu wa mwaka 2010-11 kwa madai walimchezesha kiungo Janvier Besala Bokungu katika mchezo wa kwanza uliofanyika mjini Lumbumbashi dhidi ya klabu ya Simba ya Tanzania kinyuma na taratibu za uhamisho.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo iliyo chini ya kibopa Moses katumbi imeleeza kuwa rufaa hiyo itawasilishwa FIFA na mawakili kutoka nchini Ubelgiji Luc Mission na Gregory Ernes ambapo itaambatana na vilelezo maaluma ambavyo vinaonyesha uhalali wa Janvier Besala Bokungu ambae alirejea nyumbani Kongo akitokea kwenye klabu ya Espirance ya nchini Tunisia.

CAF walishawishika kuiondoa Tp Mazembe katika michuano ya klabu bingwa baada ya kuridhishwa na rufaa iliyowasilishwa na uongozi wa klabu ya Simba ambayo ilionyesha uhalali wa Janvier Besala Bokungu kuwa mchezaji wa Espirance na si klabu hiyo ya mjini Lubumbashi ambapo mkataba wake na klabu hiyo ya nchini Tunisia ulitarajiwa kufikia kikomo mwezi June mwaka huu.

No comments:

Post a Comment