KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 1, 2011

UCHAGUZI WA URAISI WA FIFA WAWASHIWA TAA YA KIJANI.


Jaribio la chama cha soka nchini Uingereza la kutaka uchaguzi mkuu wa FIFA kusogezwa mbele limegonga mwamba kufuatia uchaguzi huo kufanyika hii leo huko mjini Zurich nchini Uswiz.

Uongozi wa chama cha soka nchini Uingereza ukiongozwa na mwenyekiti David Bernstein hapo jana uliibua hoja hiyo kwa kisingizo cha sakata la rushwa linalowakabili baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya shirikisho hilo hatua ambayo imepelekea JOSEP SEPP BLATTER kusalia pekee yake katika kinyang’anyiro cha uraisi.

Kabla ya kuanza kwa mkutano wa uchaguzi huko mjini Zurich mapema hii leo mwenyekiti wa chama cha soka nchini Uingereza David Bernstein aliwasilisha hoja hiyo mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu hatua ambayo ilipelekea kupigwa kura ya kuiafiki hoja hiyo ama la.

Sababu nyingine iliyotolewa na mwenyekiti huyo wa FA ni kutaka uchaguzi huo kuwa huru na wa haki kufuatia kuwa na mgombe mmoja ambae nae alikua anahusishwa na taarifa za madai ya rushwa kabla ya kusafishwa na kamati ya maadili ya FIFA siku mbili zilizopita.

Baada ya hapo jukumu la upigaji wa kila lilichukua mkondo wake kwa kila mjumbe aliehudhuria kwenye mkutano huo na majibu yalionyesha wazi kwamba wengi kati yao walihitaji uchaguzi huo uendelee.

Majibu yaliyosomwa mbele ya wajumbe hao yalionyesha wajumbe 172 ambao ni sawa na asilimia 75 walihitaji mkutano wa uchaguzi uendelee huku wajumbe 17 ambao ni sawa na asilimia 25 wakipingana na utaratibu huo.

No comments:

Post a Comment