KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, June 6, 2011

William Gallas AMTUHUMU Laurent Blanc.


Beki wa klabu ya Tottenham Hotspurs William Gallas amesema huenda akatangaza kustahafu soka la kimataifa kufuatia ukiritimba uliotawala katika bcnhi la ufundi la klabu hiyo ambalo kwa sasa lipo chini ya kocha mkuu Laurent Blanc.

William Gallas ametoa mustakabali huo kufuatia kushangazwa na maamuzi ya kocha huyo kushindwa kumjumuisha katika kikosi chake ambawcho kwa sasa kinaendelea na kampeni za kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2012.

Amesema maamuzi yaliyofanywa na Laurent Blanc hayamshawishi kama yana uzito mkubwa wa kitaaluma ambao umepekea kushindwa kumjumuisha katika kikosi chake ambacho mwishoni mwa juma lililopita kililazimisha matokeo ya sare ya kufungana bao moja kwa moja dhidi ya timu ya taifa ya Belarus.

Amesema hakuna beki wa kifaransa katika msimu wa mwaka 2010-11 alicheza kwa kiwango cha hali juu zaidi yake hivyo alistahili kuitwa kikosini kwa lengo la kusaidiana na wengine kwa ajili ya kufaulu mtihani wa kampeni zinazowaandama.

Hata hivyo amedia kwamba suala la kutoitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa bado linamuongezea chachu ya kuendelea kujituma katika klabu yake ya Spurs na ensdapo ukiritimba wa Laurent Blanc utaendelea atafanya maamuzi ya kujiweka pembani.

Ikumbukwe kuwa William Gallas alikua miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa iliyoshiriki kwenye fainali a kombe la dunia za mwaka 2010 ambao walishindwa kufikia malengo ya kufanya vizuri katika fainali hizo kufuatia mvutano uliokuwepo kikosini dhidi ya aliekua kocha wakati huo Raymond Domenech.

No comments:

Post a Comment