KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 19, 2011

ARSENAL WATAMBA KUTUMIA FEDHA.


Mtendaji mkuu wa klabu ya Arsenal Ivan Gazidis amesema bado hawajamaliza mpango ya kufanya usajili katika kipindi hiki cha kuelekea katika msimu mpya wa ligi ya nchini Uingereza.

Ivan Gazidis amelizungumza suala hilo kwa ajili ya kuwatoa hofu mashabiki wa Arsenal ambao wamekua wakijiuliza nini kinachofuata mara baada ya kukamilika kwa usajili wa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ivory Coast Gervinho.

Amesema bado kuna fedha ya kufanya usajili na kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili watafanya usajili wa wachezaji kadhaaa ambao tayari wameshawasilishwa kwake na meneja Arsene Wenger aliepania kumaliza ukame wa mataji uliodumu kwa misimu sita mfululizo.

Wakati huo huo Ivan Gazidis ameendelea kuelezea imani yake dhidio ya mmiliki wa klabu ya Arsenal Stan Kroenke kwa kusema amaonyesha ushirikiano mkubwa toka alipokamilisha mipango ya kununua sehemu kubwa ya hisa ya klabu hiyo.


Amesema mmiliki huyo kutoka nchini Marekani amekua na mipango madhubuti ya kuhakikisha kila jambo linakwenda kama lilivyopangwa hivyo anaamini kwa muonekano msimu ujao wa ligi kuna kila dalili za kufikia malengo ya kutwaa ubingwa wa michuano watakayo shiriki.

Stan Kroenke alikamilisha utaratibu wa kutambuliwa na viongozi wa chama cha soka nchini Uingereza FA kama mmiliki wa klabu ya Arsenal mwezi April kufuatia kununua na kumiliki zaidi ya nusu ya hisa za klabu hiyo ambapo kwa sasa anamiliki asilimia 66.64.

No comments:

Post a Comment