KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, July 25, 2011

Jose Enrique AFUMUA MAOVU YA NEWCASTLE UTD.


Beki wa pembeni wa Newcastle Utd Jose Enrique ameiponda mipango ya klabu hiyo ya kutaka kumsainisha mkataba mpya ambao utaendelea kumuweka huko Sta James Park kwa kipindi kigine.

Jose Enrique ameponda mipango hiyo kupitia ukarasa wake wa mtandao wa Twiter, huku akieleza wazi nia yake ya kutaka kuondoka na kujiunga na klabu zilizo tayari kumsajili katika kipindi hiki.

Ujumbe wa mchezaji huyo kutoka nchini Hispania unasomeka kwamba, “hakuna mipango yoyote inayoendelea dhidi yangu na kikubwa nikionacho ni kuharibu utaratibu wa kuniruhusu kuondoka na kutimiza malengo niliyojiwekea”.

Katika mahojiano na meneja wa Newcastle Utd Alan Pardew yaliyofanywa siku za nyuma na moja ya kituo cha televisheni cha nchini Uingereza, alisema wanaendelea vyema na mazungumzo ya kusaini mkataba mpya na Jose Enrique hivyo wanaamini watakamilisha mpango huo.

Jose Enrique anahusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu ay Liverpool pamoja na klabu ya Arsenal inayohaha kumsaka mrithi wa Gael Clichy aliejiunga na Man City mwanzoni mwa mwezi huu.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 25, alisajiliwa na Newcastle Utd mwaka 2007 akitokea Villareal na mpaka sasa ameshafanikiwa kucheza michezo 119 na kupachika bao moja.

No comments:

Post a Comment