KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, July 22, 2011

CARLOS TEVEZ AIBUA LINGINE MAN CITY.





Kizungumkuti cha uhamisho wa mshambuliaji kutoka nchini Argentina Carloz Tévez bado kinaendelea kupewa nafasi katika vyombo mbali mbali vya habari ulimwenguni kote, huku ikielezwa kwamba klabu bingwa duniani Inter Milan inajipanga kutuma ofa ya kutaka kumsajili huko City of Manchester.

Inter Milan wamengia katika mipango hiyo kufuatia uhusiano wa karibu uliopo kati ya Carloz Tévez na mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo ya mjini Milan Marco Branca ambae anadaiwa kutumiwa kama sehemu ya kumpata kirahisi mshambuliaji huyo.

Marafiki hao wawili wameonekana katika picha ya pamoja wakiwa mapumzikoni katika kisiwa cha Sardinia kilichopo nchini Italia, hatua ambayo inahisiwa huenda mipango ya ushawishi wa kusajiliwa huko Stadio Guissepe Meaza imeanza kuchukua mkondo wake.

Pia hiyo ya pamoja imetolewa kwenye gazeti la kila siku la nchini Uingereza liitwalo The Teleghaph ambapo mkurugenzi wa ufundi wa Inter Milan Marco Branca, ameonekana akimsalimu Carlos Tevez aliekua na mkewe mapumzikoni.

Hata hivyo taarifa hizo za ushawishi zimekanushwa vikali na mesemaji wa klabu ya Inter Milan ambapo amesema, watu hao wawili ni marafiki wa siku nyingi na kukutana kwao kisiwani Sardinia, hakuhusiani na taarifa zilizoripotiwa katika gazeti hilo.

Ikumbukwe kuwa mwezi uliopita Inter Milan walihusishwa na taarifa za kumshawishi Carlos Tevez ili aweze kujiunga nao kwa ajili ya msimu mpya wa ligi lakini raisi wa The Nerazurri Masimmo Morati alikanusha vikali taarifa hizo.

Wakati huo huo meneja wa Manchester city Roberto Mancini ameshika na kigugumizi alipoulizwa endapo Carlos Tevez ataondoka katika himaya yake ni mchezaji yupi atampa jukumu la unahodha kikosini msimu ujao.

Mancini amesema suala hilo ni gumu kulijibu kwa hivi sasa lakini kikubwa anachokifahamu kuna wachezaji wengi wenye uwezo wa kulivaa jukumu hilo ambalo ni muhimu katika kila klabu ya soka ulimwenguni kote.

Mancini pia akagusia mipango yake kwa ajili ya msimu ujao wa ligi ambapo amedhamiria kumaliza katika nafasi za juu zaidi baada ya kumaliza kwenye nafasi ya tatu pamoja na kutwaa ubingwa wa kombe la FA.

No comments:

Post a Comment