KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, July 20, 2011

CHELSEA WANG'ANG'ANA NA LUKAKU.


Chelsea wameendelea kuwa ving’anganizi katika harakati za kutaka kumsajili mshambuliaji kinda wa klabu ya Anderlecht ya nchini Ubelgiji Romelu Lukaku.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18 kwa siku kadhaa sasa amekua katika rada za kutaka kusajiliwa na klabu hiyo ya jijini London lakini imearifiwa kwamba bado kuna upinzani makali kutoka kwa washika bunduki wa Ashburton Grove Arsenal, Man city pamoja na Tottenham Hotspurs ambao wote kwa pamoja wanaiwani saini ya Lukaku.

Hii leo Chelsea wameripotiwa kutuma ofa mpya ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo aliefanikiwa kupachika mabao mawili katika timu ya taifa ya Ubelgiji ambayo ameitumikia mara kumi.

Mkurugenzi mkuu wa Anderlecht Herman van Holsbeeck amesema bado kuna safari ndefu ya kukamilishwa kwa usajili wa Romelu Lukaku na pengine huenda akaendeleza kubaki na klabu ya Anderlecht msimu ujao.

Ada ya uhamisho wa Lukaku siku za nyuma ilitajwa kuwa ni paund million 18 na mpaka sasa haijafahamika Chelsea wametua ofa ya kiasi gani ambacho kitaushawishi uongozi wa Anderlecht kumuachia kiurahisi.

No comments:

Post a Comment