KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, July 25, 2011

Ever Banega AIKANA INTER MILAN.


Ndoto za klabu bingwa duniani Inter Milan za kumpata kiungo kutoka nchini Argentina pamoja na klabu ya Valencia ya nchini Hispania Ever Banega zimeendelea kufifia kufuatia mchezaji huyo kusisitiza furaha yake huko Stadio Mestella.

Ever Banega usiku wa kuamkia hii leo alieleza wazi kwamba bado ni mwenye furaha ya kuendelea kuitumikia Valencia na hadhani kama kutakuwa na uwezekano wa kuihama klabu hiyo kwa sasa licha ya habari za kutaka kusajiliwa na Inter Milan kuendelea kushamiri.

Amesema ametangaza dhamira hiyo kutoka moyoni mwake na wala si kwa kumkwaza yoyote yule na pia amewataka mashabiki wote ulimwenguni kutomchukulia kama anaidharau ofa ya klabu hiyo ya nchini Italia.

Hata hivyo Ever Banega mwenye umri wa miaka 23 amedai kwamba Inter Milan ni klabu kubwa duniani ambayo kila mchezi ulimwenguni ana ndoto za kuitumikia klabu hiyo ya nchini Italia, lakini kwa upande wake bado anaona kuna kipindi kingine cha kusalia Stadio Mestella.

No comments:

Post a Comment