KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, July 22, 2011

Hugo Chavez ALIA NA MUAMUZI.


Raisi wa Venezuela Hugo Chavez amesema timu ya taifa lake ilifanyiwa kusudi katika fainali za mataifa ya bara la Amerika ya kusini na kupelekea kutolewa kimizengwe kwenye hatua ya nusu fainali dhidi ya timu ya taifa ya Paraguay.

Hugo Chavez ambae yupo nchini cuba akipatiwa matimabu ya saratani, amesema aliufuatilia mchezo huo akiwa nchini humo na kwa mshangao mkubwa alisikitishwa na maamuzi yaliyotolewa na muamuzi wa mchezo huo ya kulikataa bao halali lilofungwa na kikosi chake.

Amesema kiuhalali walistahili kutinga katika hatua ya fainali lakini kwa maamuzi mabovu yaliyotolewa yaliwafikisha katika changamoto ya mikwaju ya panati na kujikuta wakitupwa nje kwa kufungwa mabao matano dhidi ya matatu.

Hata hivyo ameahidi kufikia malalamiko hayo kwenye uongozi wa shirikisho la soka la bara la Amerika ya kusini (Conmebol) kwa ajili ya kumaoliza duku duku lake na kutaka waamuzi wenye maamuzi mabovu kutofumbiwa macho kwa madudu wanayoyafanya uwnajani.

Timu ya taifa ya Venezuela usiku wa kuamkia siku ya jumapili itakua uwanjani ikisa mshiondi wa tatu kwa kucheza na timu ya taifa ya Peru huku mchezo wa fainali kati ya timu ya taifa Paraguay dhdii ya timu ya taifa ya Uruguay ukitarajiwa kuunguruma usiku wa kuamkia siku ya jumatatu.

No comments:

Post a Comment