KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 19, 2011

Jerome Boateng AKIMBILIA NYUMBANI.


Mabingwa wa zamani wa nchini humo FC Bayern Munich wamekamilisha usajili wa beki Jerome Boateng akitokea Manchester City.

FC Bayern Munich wamekamilisha usajili wa beki huyo baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yao na viongozi wa Man city yaliyochukua siku kadhaa zilizopita kufuatia mtafaruku uliojitokeza baada ya Jerome Boateng kuzungumzia hadharani mipango ya kuwa tayari kucheza ligi ya nchini kwao Ujerumani.

Boateng, mwenye umri wa miaka 22, ataitumikia FC Bayern Munich kwa mkataba wa miaka minne huku ada ya uhamisho wake ukifanywa kuwa siri kufuatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi wa pande zote mbili.

Sababu kubwa iliyomkimbiza beki huyo huko City Of Manchester, ni kuchoshwa na utaratibu wa meneja Roberto Mancini wa kumchezesha kama beki wa pembeni ili hali yeye alihitaji kucheza kama beki wa kati huku sababu nyingine ni kuwekwa benchi mara kwa mara.

Akitambulishwa katika mkutano wa waandishi wa habari hii leo huko mjini Munich Jerome Boateng amesema ni furaha iliyoje kwake kurejea nyumbani na anaamini ataiwezesha klabu hiyo kufikia malengo ya kurejesha ubingwa wa nchini ujerumania mbao iliwaponyoka msimu wa mwaka 2009–10.

Nae mkurugenzi wa Bayern Munich ambae alichukua jukumu la kumtambulisha mchezaji huyo kwa waandishi wa habari Christian Nerlinger amemkaribisha klabuni hapo pamoja na kumtakia kheri katika maandalizi sambamba na wachezaji wenzake ambao wanajiandaa na msimu mpya wa ligi.

Kabla ya kusajiliwa na Man City mwanzoni mwa msimu uliopita Jerome Boateng, alikuwa akiitumikia klabu ya Humbug Fc ya nchini Ujerumani ambayo alifanikiwa kuichezea michezo 70.

No comments:

Post a Comment