KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, July 20, 2011

Luis Alberto Suarez Diaz AIPELEKEA URUGUAY FAINALI.


Timu ya taifa ya Uruguay imefanikiwa kutangulia katika hatua ya mchezo fainali kwenye michuano ya Copa Amerika inayofanyika nchini Argentina kwa mwaka huu 2011.

Timu hiyo iliyofanya maajabu katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 kule nchini Afrika kuisni kwa kukamata nafasi ya nne, imetinga fainali baada ya kuibanjua timu ya taifa ya Peru mabao mawili kwa sifuri.

Mabao hayo pekee na ya ushindi yalipachikwa wavuni na mshambuliaji wa klabu liverpool Luis Alberto Suarez Diaz katika dakika 53 na 58.

Nusu fainali ya pili ya michuano hiyo ya Copa Amerika inachezwa hii leo kati ya timu ya taifa ya Paraguay dhidi ya Venezuela mchezo utakaounguruma Estadio Malvinas Argentinas, mjini Mendoza

No comments:

Post a Comment