KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, July 20, 2011

MABAO YA UTATA MWISHO MSIMU UJAO.


Baada ya mzozo wa muda mrefu hatimae teknolojia ya kutambua mpira umevuka mstari wa golini, inatarajiwa kutambulishwa katika michezo ya ligi kuu ya soka nchini humo kuanzia msimu wa mwaka 2012/13.

Mtendaji mkuu wa chama cha soka nchini humo Richard Scudamore amesema teknologia hiyo itatambulishwa baada ya kukubaliana katika vikao vyao ambavyo vimedumu kwa kipindi kirefu kufuatia mvutano uliokuwepo miongoni mwa wajumbe.

Amesema wanaamini kutumika kwa teknojia hiyo kutamaliza mzozo wa utambuzi wa mabao yenye utata ambao yamekua yakifungwa katika michezo ya ligi ya nchini Uingereza na pengine kupelekea baadhi ya wachezaji na mameneja kuadhibiwa pale wanapolalama dhidi ya muamuzi kwa madai wameonewa.

Richard Scudamore hakuishia hapo bali aliendelea kwa kugusia bao la la Frank Lampard lililokataliwa katika fainali za kombe la dunia dhidi ya Ujerumani ambao walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao manne kwa moja.

Wakati Uingereza wakithibitisha kuanza matumizi ya teknolojia hiyo bado wajumbe wa shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA wamekua na mvutano wa kukubaliana kwa pamoja kutumika kwa kifaa hicho kwenye michezo iliyo chini ya shirikisho hilo.

No comments:

Post a Comment