KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, July 22, 2011

Roberto Mancini AJIKOSHA KWA CARLOS TEVEZ.


Bossi wa kikosi cha Manchester City Roberto Mancini amesema bado anauthamini mchango wa mshambuliaji kutoka nchini Argentina Carlos Tevez ambae kwa majuma mawili sasa amekua akihusishwa na taarifa za kutaka kuondoka huko City Of Manchester.

Robertto amncini ametoa msisitizo huo, baada ya siku mbili kupita ambazo zilishuhudia uhamisho wa Carlos tevez wa kutaka kurejea Sport Club Corinthians Paulista ya nchini Brazil ukikwama kufuatia muda wa kufanya hivyo kufikia kikomo nchini humo.

Mancini amesema bado anataka kufanya kazi na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 na wana hana hiyana dhidi yake zaidi ya kutambua nini anachokifanya akiwa uwanjani na mwisho wa siku kupata matokeo mazuri.

Amesema Carlos Tevez ni kweli anataka kuondoka klabuni hapo nay eye kama meneja alionyesha ushirikiano wa kutimiza lengo hilo, kwa kutoa ruhusa ya kuuzwa lakini imetokea bahati mbaya hivyo hana budi kumkaribisha kundini.

Carlos Tevez amekua akilazimisha kuondoka Man City kwa kigezo cha kutaka kukaa karibu na familia yake yenye watoto wawili wa kike ambayo inaishi nchini kwao Argentina.

No comments:

Post a Comment