KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, July 22, 2011

Roberto Martinez AKANUSHA UVUMI UNAOMUANDAMA NZOGBIA.


Meneja wa klabu ya Wigan Athletics Roberto Martinez amekanusha taarifa za kugoma kwa mshambuliaji wa kikosi hicho Charles Nzogbia ambae anadaiwa kukasirishwa na hatua ya kuharibiwa kwa mipango ya kutaka kusajiliwa na klabu ya Aston Villa.

Roberto Martinez amelazimika kukanusha taarifa hizo, ambazo amedai hazina ukweli wowote huku akidai kwamba Charles Nzogbia ni mwenye furaha na anaendelea vyema na maandalizi ya msimu mpya wa ligi sanjari na wachezaji wengine klabuni hapo.

Amesema mara kadhaa vyombo vya habari vimekua vikiandika na kuripoti taarifa zenye utata mkubwa kama ilivyokua na mshambuliaji huyo kutoka nchini Ufaransa hivyo hajashtushwa na kile kilichowafikia wadau wa soka ulimwenguni kote.

Hata hivyo amemsifia Charles Nzogbia kwa ujasiri alionao wa kuendelea kufanya kazi yake pasipo kujali kinachozungumzwa juu ya fununu za uhamisho zinazomkabili kwa sasa.

Licha ya kuhusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu ya Aston Villa iliyotuma ofa ya paund million 9 huko DW Stadium na kuwekwa kapuni, Charles Nzogbia pia anawaniwa na klabu ya Sunderland.

No comments:

Post a Comment