KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, July 25, 2011

SAKATA LA MLUNGULA KUENDELEA FIFA.


Mjumbe wa kamati kuu ya shirikisho la soka duniani kote Hany Abo Rida atakua mtu wa pili kusomewa shitaka la kujihusisha na masuala ya utoaji wa rushwa ndani ya shiriokisho hilo wakati wa kampeni za uchaguzi wa raisi uliofanyika mapema mwezi uliopita huko mjini Zurich nchini Uswiz.

Hany Abo Rida raia wa nchini Misri ataanza kujibu tuhuma zinazomkabili wakati wowote kuanzi sasa baada ya aliekua raisi wa shirikisho la soka barani Asia Mohamed Bin Hammam kuhukumiwa kifungo cha kutojihusisha na msuala ya soka maishani mwake.

Mjumbe huyo wa FIFA anakabiliwa na tuhuma za kuhusika katika utoaji wa mlungula, kufuatia kuwepo kwenye kundi la watu walioongozana na Mohamed Bin Hammam huko Amerika ya kati ambapo ilithibitika aliwahionga baadhi ya wajumbe wa shirikisho la soka la Caribbean.

Kesi ya Hany Abo Rida itasikilizwa sambamba na watu wengine wawikli waliokuwepo kwenye safari hiyo ambao ni Vernon Manilal Fernando wa nchini Sri Lanka pamoja na Thai Worawi Makudi.

Mohamed Bin Hammam amethibitka alitoa kiasi cha dola elfu 40 kwa baadhi ya wajumbe wa shirikisho la soka la Caribbean, ili wamuwezesha kupata kiti cha uraisi wa FIFA.

No comments:

Post a Comment