KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, July 25, 2011

SUPER MARIO BALOTELLI NA VIMBWANGA VYAKE.


Mshambulaiji wa kitaliano Mario Balotelli amekanywa vikali na meneja wa klabu ya Man city Roberto Mancini kufuatia vitendo vyake vya utovu wa nidhamua anavyoendelea kuvionyesha akiwa aktika majukumu ya kiutendaji.

Mancini amelazimika kumkanya mshambuliaji huyo mwenye sifa ya utukutu kufuatia kitendo alichokifanya katika mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Los Angles Gaklax uliochezwa alfajiri ya hii leo kwa saa za hapa nyumbani.

Mario Balotelli aliikosesha bao la wazi klabu yake kufuatia uzembe alioufanya wa kuupiga mpira wa kisigino na kutoka nje ya uwanja ili hali akiwa na nafasi ya kupachika bao la pili baada ya kupachika bao la kwanza kwa njia ya mkwaju wa penati.

Hatua hiyo ilimlazimu Mancini kumtoa nje ya uwanja, lakini bado mshambuliaji huyo aliendelea kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kutoa lugha za kukejeli huku akidai alisikia filimbi na ndio maana aliucheza mpra kwa ksigino.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Roberto Mancini amesema mshambuliaji huyo anatakiwa kuwa na nidhamu wakati wote pamoja na kujifahamu ana nafasi gani akiwa uwanjani na kwenye jamii.

Hata hivyo alivyotakiwa kuyaanisha maneno aliyokua akirushiana na Mario Balotelli mara baada ya kumtoa nje na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwingine, Mancini aligoma kufanya hivyo huku akidai kwamba muhiska alisikia kwa sababu anafahamu kitaliano.

Katika mchezo huo wa kirafiki uliochezwa nchini Marekani, Man City walichomoza na ushindi wa penati nane kwa saba, baada ya kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Los Angles Galax inayotumikiwa na kiungo kiingereza David Beckham.

No comments:

Post a Comment