KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, July 20, 2011

TERRY AMPIGIA UPATU MIDRIC.


Nahodha na beki wa kikosi cha Chelsea John Terry amesema kiungo wa klabu ya Tottenham Luka Modric anastahili kusajiliwa na The Blues.

John Terry amezungumza suala hilo akiwa mjini Kuala Lumpur ambapo amesema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 ana vigezo vyote vya kuwa miongoni mwa wachezaji wa Chelsea msimu ujao ambao wamepania kufanya kila linalowezekana kwa ajili ya kurejesha ubingwa wa Uingereza unaoshikiliwa na Man utd.

Amesema anaamini uongozi wa Chelsea bado unahangaikia suala la kumsajili Modric na imani yake yamtuma hakuna kitakacho shindiokana hasa ikizingatiwa tayari ofa yake imeshaboreshwa na kufikia kiasi cha paund million 27.

Luca Modric amekua katika wakati mgumu wa kutaka kuihama Tottenham Hotspurs kufuatia mwenyekiti wa klabu hiyo ya jijini London Daniel Levy, kumuwekea ngumu kila kukicha.

Hata hivyo jana mchezaji huyo kutoka nchini Croatia alijumuishwa kwa mara nyingine tena kikosini katika mchezo wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi dhidi ya mabingwa wa soka nchini Afrika kuisni Orlando Pirates ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

No comments:

Post a Comment