KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, July 20, 2011

TIAGO NA FILIPE MELLO WAONYESHWA MLANGO WA KUTOKEA.



Uongozi wa klabu ya Juventus umekubali kumuachia kiungo kutoka nchini Brazil Tiago na kisha utatoa ruhusa kwa mbazil mwingine Felipe Melo kuondoka klabuni hapo.

Tiago aliwahi kuvitumikia vilabu vya Benfica, Chelsea pamoja na Olympic Lyon ameonyeshwa mlango wa kutokea baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kucheza kwa kiwango msimu uliopita.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30, msimu uliopita alilazimika kupelekwa kwa mkopo nchini Hispania kunako klabu ya Atletico Madrid na alifanikiwa kucheza michezo 34 ya ligi ya nchini humo lakini bado hakuwaridhisha mabosi wake huko mjini Turine.

Kuondoka kwake mjini Turin tayari kumeshainufaisha Atletioco Madrid ambao muda mcheche uliopita wamekamilisha taratibu zoyte za kumsajili moja kwa moja.


Nae kiungo Philipe Melo aliesajiliwa kwa mbwembwe na Juventus akitokea Fiorentina mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la mabara iliyofanyika nchini Afrika kusini mwaka 2009 yu njiani kupewa taarifa za kuondoka.

Kabla hajaelezwa chochote na uongozi waThe Bianconeri, Philipe Melo ameanza kujihami kwa kusema endapo suala hilo litajitokeza atarejea nyumbani kwao Brazil kujiunga na Sao Paulo ambao wapo tayari kumsajili.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 amesema kwa sasa anataka kutuliza akili akiwa nyumbani kwao Brazil na hana mpango wowote wa kutaka kuishi barani ulaya licha ya klabu ya Paris-Saint Germain *PSG* ya nchini ufaransa pamoja na Galatasaray ya nchini Uturuki kuwa tayari kumsajili.

Mpaka sasa Philipe Mello ameshavichezea vilabu kadhaa barani Ulaya ambapo maisha yake barani humo yalianzia nchini Hispania akiwa na klabu ya Real Mallorca, Racing Santander na Almeria na kisha alihamia nchini Italia kujiunga na Fiorentina kabla ya kusajiliwa na Juventus mwaka 2009.

Na chanzo chetu cha habari dakika chache zilizopita kimetuarifu kwamba tayari Philipe Melle amepewa ruhusa ya kuondoka huko Stadio Olimpico di Torino.

No comments:

Post a Comment