KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, July 20, 2011

UHAMISHO WA JAMAA UMELALA DORO


Safari ya mshambuliaji wa kutoka nchini Argentina pamoja na klabu ya Manchester City, Carlos Tevez ya kurejea nchini Brazil imeingia gizani kufuatia uongozi wa Sport Club Corinthians Paulista kujiondoa kwenye harakati za kutaka kumsajili katika kipindi hiki.

Safari ya mshambuliaji huyo ya kurejea nchini Brazil ambayo kwa majuma mawili sasa imekua ikizunguzwa kwa mapana na marefu imefikia hapo baada ya mkutano wa wajumbe wa bodi ya Sport Club Corinthians Paulista uliofanyika usiku wa kuamki hii leo, kuafiki maazimio ya kutomsajili.

Sababu iliyopelekea kukwamisha safari ya Carlos Tevez ni muda wa uhamisho wa wachezaji huko nchini Brazil kutarajia kufikia kikomo hii leo mishale ya saa sita usiku kwa saa za nchini humo huku kukiwa hakuna muelekeo wa kuuwahi muda huo.

Raisi wa Sport Club Corinthians Paulista Andres Sanchez amesema walikua na malengo mazuri ya kumrejesha kundini mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, lakini ushirikiano dhaifu uliotolewa na uongozi wa Man City umewakatisha tamaa kwa kiasi kikubwa.

Amesema mpaka wanafikia maamuzi ya kufifisha safari ya Carlos Tevez, bado viongozi wa Man city walikua hawajathibitisha chochote juu ya kukubali kupunguza sehemu ya ada ya uhamisho wa mchezaji huyo ambayo ni paund million 40.

Sport Club Corinthians Paulista, walikua tayari wameshatuma ofa ya paund million 35, lakini ofa hiyo ilikataliwa, na kwa mshangao mkubwa siku mbili zilizofuata Man City walithibitisha kupitia kwa meneja wao Roberto Mancini wamekubali kumuuza Carlos Tevez.

Hata hivyo bado kuna uwezekano kwa mshambuliaji huyo kuondoka huko City Of Manchetster kufuatia kuwepo katika mipango ya klabu ya Juventus ya nchini Italia ambayo tayari ilishatangaza nia ya kutaka kumsajili katika kipindi hiki.

Kama itakumbukwa vyema lengo kubwa la Carlos Tevez kulazimisha safari ya kuondoka Man City lilikua ni kutaka kuwa karibu na familia yake ya watoto wawili wa kike iliopo nyumbani kwao Argentina hivyo hatua ya kujindoa kwa Sport Club Corinthians Paulista itakua imepoteza lengo lake.

No comments:

Post a Comment