KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, July 25, 2011

URUGUAY BINGWA COPA AMERICA 2011.


Timu ya taifa ya Uruguay imefanikiwa kutwaa ubingwa wa fainali za mataifa ya Amerika ya kusini *COPA AMERIKA* baada ya kuifunga timu ya taifa ya Paraguay katika mchezo wa hatau ya fainali uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo.

Uruguay ambao walitinga katika hatua hiyo baada ya kuibanjua timu ya taifa ya Peru, wametimiza lengo lao la kuwa mabingwa mwaka huu 2011, kufuatia mabao mawili yaliyofungwa na Diego Forlán Corazo pamoja na Luis Alberto Suarez Diaz aliefunga bao moja na kukamilisha idadi ya mabao matatu kwa sifiri.

Ushindi huyo wa timu ya taifa ya Uruguay, unaifanya nchi hiyo kufikisha idadi ya mataji 15 ya michuano hiyo waliyotwaa toka kuanzishwa kwake mwaka 1916.

Michuano hiyo kwa mwaka huu ilianza kutimua vumbi lake July Mosi iliyashirikisha mataifa toka a Amerika ya kusini ambayo ni

• Argentina (hosts)
• Bolivia
• Brazil (holders)
• Chile
• Colombia
• Ecuador
• Paraguay
• Peru
• Uruguay
• Venezuela

Huku Mexico na Costa Rica wakishiriki kama waalikwa kutoka Amerika ya kati.

No comments:

Post a Comment