KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 19, 2011

Valon Behrami AIPIGIA UPATU FIORENTINA.


Winga wa klabu ya Fiorentina Valon Behrami ameonyesha imani kwa kiungo wa nchini humo Alberto Aquilani kuwa atafanikiwa kubaki nyumbani licha ya kutakiwa kurejea Anfield kujiunga na kikosi cha klabu yake ya Liverpool.

Valon Behrami ameonyesha imani hiyo alipohojiwa na moja ya gazeti la michezo nchini Italia ambapo amesema Alberto Aquilani ana vihezo vya kutosha kuendelea kubaki nyumbani na kucheza katika klabu kubwa za nchini humo.

Amesema baada ya kurejeshwa Italai kwa mkopo mwanzoni mwa msimu uliopita, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 ameonyesha uwezo mzuri ambao umewavutia viongozi wa vilabu mbali mbali ikiwepo klabu ya Fiorentina.

Hata hivyo Alberto Aquilani bado ana mkataba na klabu ya Liverpool hadi mwaka 2014, hatua ambayo inaendelea kumfanya kuwa mchezaji anaefikiriwa huenda akawa kwenye mipango ya meneja wa klabu ya Liverpool King Kenny Dalglish.

Wakati huo huo klabu ya Sunderland imeripotiwa kuwa na mpango wa kutuma ofa ya kutaka kumsajili Alberto Aquilani ambae kabla ya kujiunga na Liverpool alikuwa akiitumikia klabu ya AS Roma.

No comments:

Post a Comment