KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, August 13, 2011

AL-AHLY WAKAMILISHA LENGO JIJINI CAIRO.


Mabingwa mara sita wa barani Afrika Al Ahly usiku wa kuamkia hii leo walitimiza azma yao ya kupata ushindi katika mchezo wa hatua ya makundi la ligi ya mabingwa barani humu, baada ya kuichapa Mouloudia Alger ya nchini Algeria mabao mawili kwa sifuri.

Wakicheza mbele ya mashabiki wao lukuki jijini Cairo nchini Misri Al Ahly walipata mabao hayo mawili ya ushindi kupitia kwa mshambuliaji Emad Motaeb ambae jana alionekana kuwa mwiba mkali katika ngome ya ulinzi ya Mouloudia Alger.

Ushindi huo wa mabao mawili kwa sifuri unaipa nafasi Al Ahly kufikisha point nne ambazo zinawapa uwezo wa kufufua matumaini yao ya kutimiza malengo ya kutaka kutinga katika hatua ya nusu fainali.

Maneja wa Manuel Jose amesema licha ya kupata ushindi huo mzuri bado wapinzani wao walionyesha soka safi na lenye upinzani mkubwa hali ambayo ilimpa hofu ya kudhani huenda matokeo yangebadilika kabla ya dakika 90 kumalizika.

No comments:

Post a Comment