KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 22, 2011

Alberto Aquilani APIGIWA UPATU WA KUREJEA NYUMBANI.

Mabingwa wa soka nchini Italia AC Milan wametangaza mikakati ya kutaka kumrejesha nyumbani kiungo wa klabu ya Liverpool Alberto Aquilani, ambae kwa sasa ana wakati mgumu wa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha King Kenny Dalglish.

Mikakati ya kusajiliwa kwa kiungo huyo ambae kabla ya kusajiliwa na Liverpool alikua akiitumikia AS Roma, imetangazwa na raisi wa Ac Milan Silvio Berlusconi ambae amepata msukumu mkubwa kutoka kwa meneja wake Massimiliano Allegri.

Akikariwa na gazeti linalotoa habari za michezo nchini Italia liitwalo Gazzetta dello Sport Silvio Berlusconi amesema wamejipanga vyema katika harakati za kutaka kumsajili kiungo huyo na wanaamini kila kitu kitakwenda vizuri kabla ya August 31.

Amesema meneja wa kikosi cha AC Milan Massimiliano Allegri, amemueleza namna gani alivyokua na hamu ya kutaka kumuona Alberto Aquilani, anakuwa katika mipango yake msimu huu ambao utashuhudia wakiwa na mipango madhubuti ya kutaka kutetea ubingwa wa Scudetto.

Hata hivyo Alberto Aquilani, bado ana mkataba na klabu ya Liverpool hadi mwaka 2014, na msimu uliopita alipelekwa kwa mkopo katika klabu ya Juventus baada ya kutokuwepo kwenye mipango ya aliekua meneja wa Liverpool Roy Hodgson.

Katika hatua nyingine AC Milan wametangaza mipango ya kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Fiorentina Riccardo Montolivo.

No comments:

Post a Comment