KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 26, 2011

Alberto Aquilani KUREJEA NYUMBANI KWAO ITALIA.

Majogoo wa jiji Liverpool wamethibitisha taarifa za kumruhusu kiungo wao kutoka nchini Italia Alberto Aquilani kuondoka kwa mkopo na kurejea nyumbani kwa mara nyingine tena kujiunga na mabingwa wa Sirie A AC Milan.

Liverpool wamethibitisha taarifa hizo kwa kuonyesha ni vipi walivyotayari kufanya hivyo kutokana na mazungumzo yaliyokua yanaendelea siku tatu zilizopita baina yao pamoja na wakala wa kiungo huyo sanjari na viongozi wa AC Milan.

Kuondoka kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, kutainufaisha Liverpool kupata kiasi cha Euro million 6 ambazo ni sawa na paund million 5.3, endapo Ac Milan watakua tayari kukamilisha dili ambalo lipo wazi.

Mkurugenzi wa michezo wa Liverpool Damien Comolli amesema utaratibu wa kuuzwa kwa mkopo kwa kiungo huyo, wanaamini utaendelea kumjenga kiushindani kutokana na uhalisia wa kikosi chao kwa sasa ambao haumpi nafasi ya kucheza kila juma.

Msimu uliopita Alberto Aquilani, alijiunga na Juventus kwa mkopo kufuatia kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Liverpool ambacho kilikua chini ya meneja Roy Hodgson ambae alirithi mikoba ya Rafael Benitez.

Alberto Aquilani, alisajiliwa na Liverpool mwaka 2009 akitokea AS Roma kwa ada ya uhamisho wa paund million 20.

No comments:

Post a Comment