KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 10, 2011

Arda Turan ASAJILIWA MJINI MADRID.


Atletico Madrid wamekubali kumsajili winga kutoka nchini Uturuki na klabu ya Galatasaray Arda Turan kwa mkataba wa miaka minne.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 24, ataondoka nchini Uturuki mwishoni mwa juma hili kuelekea mjini Madrid tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha masuala ya usajili wake.

Arda Turan kesho atakutana na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa taarifa za kuwaaga mashabiki wake pamoja na wale wa Galatasaray sambamba na kuwashukuru kwa ushirikiano waliompa kwa kipindi cha miaka sita alichoishi huko Türk Telekom Arena.

Tayari Arda Turan ameshaingizwa katika mipango ya meneja mpya wa Atletico Madrid Gregorio Manzano na atajumuishwa kwenye kikosi kitakachocheza mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya ligi ya barani ulaya juma lijalo dhidi ya klabu ya Vitoria Guimaraes ya nchini Ureno.

Televisheni ya taifa ya nchini Uturuki imeripoti kuwa Atletico Madrid wamekubalia kumsajili winga huyo kwa ada ya uhamisho wa Euro million 12.

No comments:

Post a Comment