KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 24, 2011

ARSENAL KUPENYA HII LEO?

Kitendaiwili cha washika bunduki wa Ashburton Griove Arsenal, cha kucheza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, hii leo kinatarajia kuteguliwa pale klabu hiyo itakaposhuka huko Stadio Friuli, nchini Italia kupambana na Udinese Calcio katika mchezo wa pili wa hatua ya mtoano.

Arsenal wameelekea nchini Italia huku wakiwa katika hali ya kuweweseka na matokeo ambayo hayaridhishi toka mwanzoni mwa msimu huu amnbapo mpaka sasa wameshafanikiwa kupachika bao moja ambalo lilipatikana katika mchezo wa kwanza uliowakutanisha na Udinese Calcio.

Katika mchezo wa hii leo Arsenal watamtumia mshambuliaji na nahodha wao Robin Van Parsie, ambae hakujumuishwa kikosini kwenye mchezo wa kwanza kufuatia adhabu ya kufungiwa mchezo mmoja aliyoangushiwa na shirikisho la soka barani ulaya UEFA.

Arsenal pia itakua ikichagizwa na kurejea kwa meneja wao Arsene Wenger katika benchi la Ufundi, baada ya kukaa jukwaani katika mchezo wa kwanza ambapo hata hivyo alizusha kizaa zaa cha kuwasiliana na vbenchi la ufundi na kulazimika kufungiwa michezo mingine miwili na UEFA.

Kufuatia maombi yaliyowasilishwa jana na uongozi wa Arsenal ya kutaka kucheleweshwa kwa adhabu hiyo, kunamfanya mzee huyo wa kifaransa kurejea katika majukumu yake ya kikazi hii loe.

Akiwa katika mkutano na waandishi wa habari Arsene Wenger amesema hawaidharau Udinese Calcio, zaidi ya kutambua uwezo wao wanapokua uwanjani, hivyo atahakikisha anawahimiza wachezaji wake kucheza kwa kujituma wakati wote.

Arsene Wenger pia akagusia suala la kuwapa nafasi wachezaji wenye umri mdogo katika kikosi chake ambapo amedai kwamba amelazimika kufanya hivyo kufautia kuona umuhimu wao.

Nae beki wa pembeni wa Arsenal Bakari Sagna, amesema bado kikosi chao kipi vizuri licha ya kuwapoteza wachezaji nyota kama Cesc Fabregas pamoja na Samir Nasri amnbao wameondoka kikosini katika kipindi hiki na kujiunga na klabu zilizowasajili.

No comments:

Post a Comment