KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 5, 2011

ARSENAL MIKONONI MWA WATALIANO.


Hatimae shirikisho la soka barani Ulaya UEFA hii leo limepanga ratiba ya mwisho ya michezo ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kabla ya kuanza kwa hatua ya makundi mwezi ujao katika viwanja mbali mbali barani humo.

UEFA wamekamilisha hatua ya upangaji wa michezo hiyo ya mtoano mjini Nyon nchini Uswiz ambapo washika bunduki wa Ashburton Grove Arsenal waliomaliza katika nafasi ya nne msimu uliopita kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza wameanguka mikononi mwa Udinese toka nchini Italia.

Arsenal wameangukia mikonini mwa klabu hiyo ambayo pia ilimaliza katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi nchini Italia, na kujikuta ikifuzu kucheza hatua ya mtoano ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa mwaka 2011-12.

Udanise wamepangwa na Arsenal huku kikosi chao kikiwa na mapungufu makubwa baada ya kuuzwa kwa wachezaji nyota katika kipindi hiki kama Alexis Sanchez aliesajiliwa na FC Barcelona, Gokhan Inler aliejiunga na Napoli pamoja na Cristian Zapata aliesajilia na Villareal.

Mchezo wa kwanza wa vilabu hivi viwili utachezwa jijini London kati ya August 16 ama 17 na kisha mchezo wa pili utapigwa nchini Italia kati ya August 23 ama 24.

Kabla ya kupangwa kwa ratiba hiyo Arsenal walikua na uwezekano mkubwa wa kukutana na FC Zurich, FC Twente, Odense ama Rubin Kazan, lakini mambo yamekwenda tofauti na vile ilivyokua inafikiriwa.

Mkurugenzi mkuu wa Udanise aliehudhuria katika hafla ya upangaji wa ratiba ya michezo hiyo ya mtoano Franco Collavini amesema wameipokea kwa mikono miwili ratiba iliyotolewa na watahakikisha wanajitahidi kucheza kwa kujituma ili kupata nafasi ya kutinga katika hatua ya makundi.

Hata hivyo Franco Collavini amekiri kupangwa na klabu kubwa barani Ulaya ambapo amesema bado inawapa changamoto kubwa ambayo itawasaidia kupima uwezo wa kikosi chao.
Michezo mingine ya hatua ya mtoano iliyopangwa hii leo ni pamoja na:

Wisla Krakow (Poland) v APOEL (Cyprus)

Maccabi Haifa (Israel) v Genk ( Ubelgiji)

Dinamo Zagreb (Croatia) v Malmo (Sweden)

FC Copenhagen (Denmark) v Viktoria Plzen (Jamuhuri Czech)

BATE Borisov (Belarous) v Sturm Graz (Austria)

LEAGUE ROUTE:

Odense (Denmark) v Villarreal (Hispania)

FC Twente(Uholanzi) v Benfica (Ureno)

Bayern Munich (Ujerumani) v FC Zurich ( Uswiz)

Olympic Lyon (Ufaransa) v Rubin Kazan (Urusi)

No comments:

Post a Comment