KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, August 13, 2011

ARSENE WENGER AMKANA JUAN MATA.

Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ameonyesha hali ya kutokua tayari kumsajili kiungo kutoka nchini Hispania pamoja na klabu ya Valencia Juan Mata ambae siku za hivi karibuni alihusishwa sana na taarifa za kutaka kuelekea jijini London kujiunga na washika bunduki hao.

Arsene Wenger amesema hawajatuma ofa ya kutaka kumsajili kiungo huyo na bado anaendelea kushangazwa na taarifa zinazotolewa kwenye baadhi ya mitandao barani Ulaya ambayo inadai kwamba yeye binafsi yu katika mstari wa mbele kutaka kumsajili.

Amesema hakuna asiefahamu Juan Mata ni mchezaji mzuri na mwenye sifa ya kukitumikia kikosi chake, lakini, hatawasilisha maombi ya kutaka kumsajili katika kipindi hiki, hivyo amewataka mashabiki wa Arsenal kuwa watulivu katika suala hilo.

Katika hatua nyingine Arsene Wenger amekanusha taarifa za klabu ya Arsenal, kuwa karibu kumsajili kiungo kutoka nchini Brazil pamoja na klabu ya Shakhtar Donetsk J√°dson Rodrigues da Silva.

Mbali na wachezaji hao Arsenal bado wanendelea kuhusishwa na taarifa za kutaka kuwasajili baadhi ya wachezaji kama winga kutoka nchini Ghana na klabu Olympic Marseille Andre Ayew na kiungo wa klabu ya Sochaux Marvin Martin.

Wengine ni mabeki Christopher Samba wa Blackburn Rovers, Scott Dann wa Birmingham city, Gary Cahill wa Bolton Wanderers pamoja na Phil Jagielka wa Everton.

Wakati huo huo uongozi wa klabu wa klabu ya Arsenal umeutaka uongozi wa Manchester City kukubalia dili la kumpeleka jijini London mshambuliaji kutoka nchini Argentina Carlos Tevez kama sehemu ya kubadilishana na kiungo kutoka nchini Ufaransa Samir Nasri.

Arsenal wamewasilisha ombi hilo huku wakionyesha kuwa tayari kumuachia Samir Nasri aligoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia The Gunners ambayo pia imeshakubali kumuachia Fabregas alie njiani kurejea nyumbani kwao Barcelona nchini Hispania.

Dili hilo linaonekana kuwa katika hali ta mtego zaidi, kufautia ada ya Samir Nasri kutangazwa kuwa ni paund million 22, ili hali ada ya uhamisho wa mshambuliaji Carlos Tevez ni paund million 45.

Carlos Teves tayari ameshaonyesha nia ya kutaka kuondoka Etihad Stadium katika kipindi hiki, huku akieleza wazi amechoshwa na mazingira ya mji wa Manchester sambamba na kuhitaji kukaa karibu na familia yake yenye watoto wawili wa kike iliyo nchini Argentina.

No comments:

Post a Comment