KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 29, 2011

ARSENE WENGER NA KICHAPO CHA 8-2.

Siku moja baada ya ushindi mnono wa mabao manane kwa mawili dhidi ya washika bunduki wa Ashburton Grove Arsenal, meneja wa Man Utd Sir Alex Ferguson amemkingia kifua meneja wa Arsenal Arsene Wenger kwa kusema hastahili kulaumiwa.

Sir Alex Ferguson amesema Wenger ameifanyia makubwa Arsenal na kufungwa kwake katika mchezo wa jana isiwe sababu ya kila mmoja kumnyooshea kidole kwa kisingizio cha kumtaka aachie ngazi.

Amesema huenda mashabiki wengi wamesahau nini Arsene Wenger amekifanya ndani ya klabu hiyop ya kaskazini mwa jiji la London na pengine hasira za kupoteza mchezo wa jana zinachangia kutoa lawama, lakini akawakumbusha kwa kusema ni mengi na makubwa ambayo mzee huyo kutoka nchini Ufaransa ameyafanya na kuifaidisha klabu.

Hata hivyo Sir Alex Ferguson, amekirui kushangazwa na matokeo yaliyopatikana licha ya kubainisha wazi kwamba Arsenal walikua na nafasi finyu ya kuondoka na furaha huko Old Trafford katika mchezo huo.

Amebainisha wazi kuwa, kikosi cha Arsenal kilikua na mapungufu makubwa ambayo yalisababishwa na sababu mbali mbali na hatua hiyo ilimpa nafasi ya kuamini ushindi upo lakini si kwa kiasi kikubwa cha mabao kama kilichotokea.

Wakati huo huo:

Arsene Wenger amekataa kata kata kujiuzulu nafasi yake ndani Arsenal huku akidai kwamba hakuna sababu ya kufanya hivyo ili hali anaona kuna nafasi ya kuendeleza mazuri licha ya kichapo walichokipokea hiyo jana.

Arsene Wenger amesema ni vigumu kuchukua maamuzi hayo, kutokana na na muda uliopo ambao anaamini utamuwezesha kufanya marekebisho wa kutosha na kurejea katika reli ya ushindi.

Amesema kichapo cha mabao manene kwa moja kimemuuma yeye binafsi na kila mmoja anaeshabikiwa Arsenal kitakuwa kimemuuma, na hivyo hatua hiyo inampa nafasi ya kufungua ukurasa mwingine wa kutazamna namna gani anaweza kuirejesha Arsenal yenye ushindani.

Hata hivyo Arsene Wenger amemtaka radhi yoyote yule anaehusika na klabu hiyo ulimwenguni kote kwa kusema, anastahili kufanya hivyo kutokana na kile kilichoonekana huko Old Traffold.

Nao uongozi wa klabu ya Arsenal umetoa ofa ya kuingia bure uwanjani katika mchezo ujaoa mbapo The Gunner watakua nyumbani wakiwakaribisha Swansea.

Ofa hiyo imechukuliwa kama sehemu ya kuomba radhi kwa mashabiki wote ambao kwa hakika wameumizwa na kipigo cha mabao manene kwa mawili.

Katika hatua nyingine meneja wa zamani wa klabu ya Arsenal George Graham, amesema anaamini kikosi cha Arsenal kitarejea katika makali yake lakini si kwa kusaka ubingwa bali ni kwa kusaka namna ya kumaliza katika nafasi nne za juu.

Arsenal haijawahi kufungwa idadi kubwa ya mabao kama ilivyokua katika mchezo wa jana toka mwaka 1896.