KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 19, 2011

AS ROMA YANUNULIWA!

Hatimae klabu kongwe nchini humo Associazione Sportiva Roma *AS ROMA* imeuzwa kwa mfanyabiashara kutoka nchini Marekani Thomas Di Benedetto anaemiliki kampuni za uwekezaji zilizopo mjini Boston.

Thomas Di Benedetto amekamilisha azma hiyo ya kuinunua klabu AS ROMA baada ya mpango wake kusitishwa mwezi wa nne kufuatai sababu ambazo zilikwamishwa na viongozi wa klabu hiyo ya mjini Roma.

Hata hivyo hatua ya kununuliwa kwa klabu ya AS Roma na muwekezaji huyo imepitia katika mpango wa kukunua hisa za wawekezaji wengine kwa makubaliano maalum ambao walikua wakizihodhi siku za nyuma.

Thomas Di Benedetto, ametuamia kiasi cha paund za kiingereza million 52.2 ambazo ni sawa na euro million 60, kwa ajili ya kunua asilimia 60 ya hisa za klabu hiyo ambazo zinampa madaraka ya kuwa msemaji wa mwisho katika bodi ya wawekezaji.

Kufuatia hatua hiyo As Roma inakua klabu ya kwanza kumilikiwa na muwekezaji wa kigeni ambae anamiliki asilimia kubwa ya hisa.

No comments:

Post a Comment