KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 4, 2011

BABU AAGWA RASMI NCHINI UHOLANZI.Kipa shujaa wa nchini humo Edwin van der Sar jana aliagwa rasmi katika medani ya soka kwa kuchezwa mchezo maalum uliowashirikisha wachezaji aliocheza nao toka enzi za ujana wake.

Mchezo huo ulihudhuriwa na mashabiki 53,000 ambao wote kwa pamoja alitumia muda wao kumpa mkono wa kwa heri huku wengine wakiomnyesha mapenzi dhidi kipa huyo mwenye umri wa miaka 40 kwa kumwaga machozi.

Mchezo huo ulivishirikisha vikosi viwili tofauati ambavyo vyote vilitumikiwa na Edwin van der Sar ambapo kikosi cha kwa kwanza kukichezea kiliwajumuisha wachezaji wa zamani waliocheza timu ya taifa ya Uholanzi pamoja na klabu ya Ajax ambao ni Patrick Kluivert, Marc Overmars, Frank Rijkaard, Frank de Boer, Ronald de Boer, Devis Bergkamp pamoja na Giovanni van Bronckhorst.

Kikosi cha pili kiliitwa, Van der Sar's Dream team, ambacho kiliwajumuisha marafiki wa kipa huyo ambao ni Wayne Rooney, Ryan Giggs, Dirk Kuyt, Edgar Davids, Rio Ferdinand, nemanja vidic, Rio Ferdinand pamoja na Dennis Bergkamp ambae alifunga bao la ushindi.

Edwin van der Sar alianza kutambulika katika medani ya soka la kimataifa akiwa na umri wa miaka 19, na hii ilikua mwaka 1990 akiitumikia klabu ya Ajax Amsterdam na mwaka 1999 aliihama klabu hiyo na kuelekea nchini Italia kujiunga na Juventus aliyoitumikia hadi mwaka 2001.

Baada ya hapo kipa huyo alielekea nchini Uingereza baada ya kusajiliw ana Fulhama FC ambapo alidumu Croven Cottege hadi mwaka 2005, na kisha alijiunga na Man Utd aliyoichezea kwa miaka sita kabl ya kutangaza kukaa pembeni Mwezi May mwaka huu.

Edwin van der Sar, ameitumikia timu ya taifa ya uholanzi katika michezo ya 130 na mara ya kwanza aliitwa kikosini mwaka 1995 na alitangaza kustahafu sola la kimataifa mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment