KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 12, 2011

Barrister Chris Green ATAMBA NIGERIA BINGWA.


Mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya shirikisho la soka nchini Nigeria, Barrister Chris Green amesema timu ya taifa ya vijana ya Nigeria chini ya umri wa miaka 20 itafika katika mchezo wa fainali na kutwaa ubingwa wa dunia mnamo August 20.

Green ametoa tambo hizo hii leo alipokutana na waandishi wa habari mjini Bogota nchini Colombia zikiwa zimepita siku mbili baada ya timu ya taifa ya Nigeria kutinga katika hatua ya robo fainali kufuatia ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya taifa ya Uingereza.

Amesema walikwenda nchini Colombia kushindana na wanaamini kila jambo linaloendelea huko limetokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya kabla ya kuanza kwa fainali za dunia za vijana ambazo miaka miwili iliyopita zilichezwa nchini Misri na timu ya taifa ya Ghana kutwaa ubingwa.

Lakini pamoja na kutoa tambo hizo Barrister Chris Green akakiri kuwepo kwa ushindani mkubwa kwenye michuano hiyo lakini akaendelea kusisitiza jambo la kukiamini kikosi cha Nigeria ambacho kitarejea tena uwanjani kupambana na Ufaransa katika hatua ya robo fainali August 14.

Kwenye michuano hiyo timu ya taifa ya Nigeria ilifanikiwa kucheza hatua ya pili baada ya kuongoza kundi la nne kwa kuwa na point tisa na mpaka hii leo wanasubiri kwenda kucheza mchezo wa robo fainali tayari wameshapachika mabao 13.

Nigeria ndio taifa pekee la barani Afrika lililosalia katika fainali hizo za kombe la dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, baada ya kuondolewa kwa mataifa kama Misri, Mali pamoja na Cameroon.

No comments:

Post a Comment