KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, August 13, 2011

Benni McCarthy ATOA SALAMU KWA MASHABIKI BONDENI.


Mshambuliaji mpya wa Orlando Pirates Benni McCarthy usiku wa kuamkia hii leo alitoa salamu kwa mashabiki wa klabu hiyo kufautia kupachika moja ya mabao yaliyowapa ushindi dhidi ya Black Leopards.

Benni McCarthy alieamua kurejea nyumbani Afrika kusini baada ya kufungashiwa virago huko barani Ulaya alipoklua akiitumikia klabu ya West ham utd ya nchini Uingereza, alianza kuonekana akiwa amevaa jezi ya Orlando Pirates, katika mchezo huo ambao uliashiria kufunguliwa kwa ligi ya PSL.

Akizungumza mara baada ya mpambano huo kumalizia katika uwanja wa Peter Mokaba mshambuliaji huyo amesema ni furaha sana kwake kutimiza malengo ya kuwazadia mashabiki wa Orlando bao ambalo limeifanya klabu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.

Hata hivyo amedai kuwa, kuanza vizuri kuna maanisha mengi mazuri yanafuata hivyo amewataka mashabiki wa The Bucs kuwa watulivu na kumuonyesha ushirikiano wa kutosha.

Ushindi wa mabao mawili kwa sifuri unaifanya Orlando Pirate kupata point tatu muhimu katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Afrika ya kusini ambayo hii leo imeendelea tena kwa michezo mingine miwili ambapo.

Free State Stars 1-1 SuperSport United - Goble Park
Platinum Stars 2-0 Ajax Cape Town - Royal Bafokeng Stadium

Michezo minghine itakayochezwa saa kadhaa zijazo ni:
Golden Arrows v Bloem Celtic - King Zwelithini Stadium
Kaizer Chiefs v Jomo Cosmos - FNB Stadium

No comments:

Post a Comment