KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 25, 2011

BIFU LA Sir Alex Ferguson NA BBC LAFIKIA TAMATI.

Hatimae mzozo kati ya meneja wa Man utd Sir Alex Ferguson dhidi ya shirika la utangazaji la nchini Uingereza BBC, umefikia kikomo baada ya kudumu kwa kipindi cha miaka saba iliyopita.

Mzozo huo umefikia kikomo baada ya pande hizo mbili kukutana na kumaliza tofauti zilizopo, ambazo zilipelekea Sir Alex Ferguson kugoma kuzungumza na shirika hilo la habari juu ya suala linalomuhusu yeye binafsi pamoja na yale yaliyokua yakiihusu klabu ya Man Utd.

Mkutano wa suluhisho umefanyika hii leo ambapo upande wa BBC uliwakilishwa na mkurugenzi wake mkuu Mark Thompson pamoja na mkurugenzi wa shirika hilo kanda ya kaskazini mwa nchini Uingereza Peter Salmon.

Kwa mantiki hiyo sasa meneja huyo kutoka nchini Scotland ataanza kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kufanyiwa mahojiano na BBC na pengine kuzungumzioa masuala yake binafsi pale itakapohitajika, huku shughuli hiyo ikitarajia kuanza mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa ligi dhidi ya Arsenal watakaosafiri hadi mjini Manchester.

Mzozo kati ya pande hizo mbili ulianza mwaka 2004, baada ya BBC kurusha kipindi kilichomzungumza vibaya mtoto wa Sir Alex Ferguson kwa kumtuhumu alikua akifanya makosa kwa makusudi katika shughuli zake za uwakala huku akitumia kivuli cha baba yake.

Hatua hiyo ilimchukiza Sir Alex Ferguson na kufikia maamuzi ya kutofanya mazungumzo na chombo chochote cha habari kilicho chini ya BBC.

No comments:

Post a Comment