KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 11, 2011

BOLTON WAANZA SAFARI YA KUMSAKA PHILIPS.Meneja wa Bolton Wanderes Owen Coyle amesema hii leo wameanza mazungumzo na viongozi wa Man City kwa ajili ya kumsajili winga kutoka nchini Uingereza Shaun Wright-Phillips ambae amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza huko Etihad Stadium.

Owen Coyle amesema mazungumzo hayo yameanza huku akiamini kumpata winga huyo ambae bado ana uwezo mkubwa wa kucheza soka licha ya kukaa nje kwa kipindi kirefu katika kikosi cha Roberto Mancini.


Amesema Shaun Wright-Phillips ni mchezaji anapendezwa nae kutokana na juhudi anazozionyesha akiwa uwanjani hivyo anaamini atamsaidia katika mtiririko wa michezo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambayo itashuhudia Bolton wakifungua dhidi ya Queens Park Rangers.

Hata hivyo amedai kwamba kwa sasa anasubiri majibu ya mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambayo amesema hana shaka nayo.

No comments:

Post a Comment