KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 4, 2011

CANTONA AWASEMEA MBOVU TEVEZ NA BALOTELLI.

Mshambuliaji wa kimataiufa toka nchini Argentina Carlos Tevez ataukosa mchezo wa kuwnai ngao ya hisani utakaochezwa mwishoni mwa juma hili katika uwnaja wa Wimbley jijini London kati ya Man City dhidi ya mahasimu wao wa kubwa Man Utd.

Carlos teves ataukosa mchezo huo kufuatia kuongezewa muda wa mapumziko na meneja wa Man city Roberto Mancini, ambapo ahatua hiyo itamfanya kurejea Etihad Stadium mapema siku ya jumapili.

Hapo awali mshambuliajui huyo mwenye umri wa miaka 27, alipewa ruhusa ya kupumzika, baada ya kumaliza majukumu la kitaifa kwenye fainali za mataifa ya Amerika ya kusini COPA AMERIKA ambapo kwa kipindi chote cha mapumziko alikua kisiwani Sardinia nchini Italia na familia yake yenye watoto wawili wa kike.

Kwa mantiki hiyo sasa Carlos Teves huenda akacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza mwishoni mwa juma lijaloa mbapo Man city wataanza nyumbani Etihad Stadium kwa kucheza na Swansea FC.

Wakati huo huo nahodha na mshambuliaji wa zamani wa mashetani wekundu Man Utd, Eric Cantona ameonyesha kuchukizwa na kauli zilizotolewa na washambuliaji wa klabu pinzani ya Man City Carlos Tevez na Super Mario Balotelli za kutopendezwa na mazingira ya mji wa Manchester.

Eric Cantona ambae kwa sasa yupo mjini Manchester tayari kwa mchezo maalum wa kumuaga aliekua kiungo wa Man utd Paul Scholes, amesema mpaka sasa haelewi sababu zilizopelekea washambuliaji hao wawili kutoa kauli hizo ambazo zinaweza kuwaharibu wachezaji yoso.

Amesema nidhamu ya wachezaji hao inategemea ni wapio wametoka, bila kutaja miji yao lakioni kwa upande wake akaeleza kwamba alipendezwa sana na mazingira ya mji wa Manchester.

Katika hatua nyingine Eric Cantona amesifia juhudi zinazofanywa na uongozi wa klabu ya Man City ambazo zina malengo ya kubadili mfumo wa uchezaji wa soka ndani ya klabu hiyo ambayo kwa sasa ina sura mpya za wacheza wenye uwezo mkubwa duniani.

Hata hivyo bado akatoa ushauri kwa viongozi hao kuhakikisha wanawaendeleza vijana chipukizi ili kuepuka suala la kutumia fedha nyingi za usajili siku za usoni kama ilivyo sasa ambapo Man city imeshatumia zaidi ya paund million 300.

Cantona hakuishia hapo bali aliendelea kuzungumzia upande wa pili kwa kumwagia sifa kede kede meneja wa Man utd Sir Alex Ferguson ambapo amesema ni meneja mwenye vigezo vya kipekee na kustahili heshima kwa kila mmoja wao.

Amesema meneja huyo kwa kipindi kirefu amekuwa na msimamo tofauti ambao unampa mafanikio bila kukiyumbisha kikosi chake, hatua mabyo inamfanya yeye kama mwanafunzi wake kumuheshimu siku hadi siku.

Amesema wachezaji wengi wazuri wameitumikia Man utd chini ya Sir Alex Fergoson na ulipofika wakati waliondoka, lakini hakuna hata siku moja kikosi cha mzee huyo kiliyumba eti kwa kisingizio cha kuondoka kwa Fulani.

Hata hivyo akadai kwamba kuondoka kwa babu huyo kutakua na shughuli nzito ya kuziba nafasi yake ambapo kwa upande wake bionafsi ameshindwa kusema yeye anampendekeza nani kuwa mbadala wa Sir Alex Ferguson.

No comments:

Post a Comment