KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 11, 2011

Christian Nerlinger AJIBU MAPIGO KWA MASHABIKI.


Mkurugenzi wa michezo wa mabingwa wa zamani wa nchini humo Bayern Munich Christian Nerlinger amesema hawajashtushwa na kichapo cha bao moja kwa sifuri walichokipokea kutoka kwa Borussia Moenchengladbach mwishoni mwa juma lililopita.

Christian Nerlinger ametoa kauli hiyo kufuatia malalamiko mengi yanayotolewa na wadau wa soka nchini Ujerumani ambao wameponda muenekano wa kikosi cha Bayern Munich huku wakidai hakina sifa ya kufungwa katika mchezo wa ufunguzi wa ligi ya nchini humo tena na klabu kama Borussia Moenchengladbach.

Amesema kupoteza mchezo wa kwanza katika ligi, kwao wanachukuliwa kama sehemu ya changamoto ambayo itawafanya kujipanga vyema kabla ya kurejea tena uwanjani mwishoni mwa juma hili kuendelea na kampeni za kusaka ubingwa wa Bundersiliga.

Christian Nerlinger pia masisitiza jambo la kukiamini kikosi cha Bayern Munich sanjari na meneja wake Jupp Heynckes kwa kusema anakipa nafasi ya kutwaa ubingwa katika msimu huu wa ligi.

Mwishoni mwa juma hili Bayern Munich wanarejea tena uwanjani kuzisaka point tatu muhimu ambapo watacheza na VFL Wolfsburg huku meneja Jupp Heynkes akikabiliwa na mzigo mzito wa kuwarejesha wachezaji wake katika hali tofauti baada ya kutoka katika majukumu ya kitaifa.

No comments:

Post a Comment