KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 8, 2011

Dickson Etuhu KATIKA BIFU ZITO SAMSON SIASIA.


Kiungo wa klabu ya Fulham Dickson Etuhu, ametangaza kujiondoka kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria ambacho kesho kitacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Ghana huko nchini Uingereza katika uwanja wa Vicarage Road.

Dickson Etuhu ametangaza kujiondoa katika timu hiyo huku akieleza wazi kwamba haweezi kuitumikia Super Eagles, ikiwa chini ya kocha wa sasa Samson Siasa.

Hata hivyo bado haijafahamika sababu ni ipi kwa mchezaji huyo kufikia hatua ya kutangaza hivyo, hali ambayo imeendelea kuchakata vichwa vya mashabiki wengi nchini Nigeria na pengine barani Afrika kwa ujumla.

Kwa mara ya kwanza Samson Siasia alimuita Etuhu kwenye kikosi chake mwanzoni mwa mwaka huu lakini kiungo huyo alitangaza kujiondoa kwa sababu za kuwa majeruhi.

Kikosi cha Nigeria kinakwenda kucheza mchezo wa kesho bila ya kuwa na wachezaji wake muhimu ambapo wengi wao ni majeruni na hawakuitwa kikosini kwa ajili ya kuivaa timu ya taifa ya Ghana.

Miongoni mwa wachezaji hao ni kipa Vincent Enyeama, mshambuliaji Ekigho Ehiosun, kiungo Fegor Ogude pamoja na beki Efe Ambrose.

Nigeria watautumia mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Ghana kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2012 ambapo watacheza na Madagascar mwezi September, na Ghana watacheza dhidi ya Swaziland.

No comments:

Post a Comment