KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 5, 2011

DILI LA FABREGAS LAKWAMA KWA MARA YA TATU !!


Matumaini ya mabingwa wa soka barani ulaya Fc Barcelona ya kumnyakua kiungo na nahodha wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas kwa ada ya uhamisho wa paund million 35, yamegonga mwamba kufuatia ofa ya klabu hiyo ya Catalunya kuwekwa kapuni.

FC Barcelona walituma ofa hiyo ya paund million million 35, baada ya ofa ya paund million 33 iliyoopngezwa kutoka paund million 27 kukataliwa na washika bunduki hao ambao wanahitaji mzigo wa paund million 40.

Arsenal wameendelea kushikilia msimamo huo, huku ikisemekana muwekezaji mwenye hisa kubwa klabuni hapo Stan Kroenke akiwa chanzo cha kusisitiza msimamo ambao unadaiwa katu hautobadilika mpaka hapo mambo yatakapowekwa sawa kama kweli Fc Barcelona wanamuhitaji Fabregas.

Kufuatia hatua hiyo sasa Fc Barcelona watatakiwa kutuma ofa nyingine kabla ya August 16 ama 17 ambapo Arsenal watakuwa wanakwenda katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa ligi ya mabingwa barani ulaya na huenda wakamtumia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24.

Hata hivyo inadaiwa kwamba Cesc Fabregas tayari ameshamueleza meneja Arsene Wenger juu ya kutokuwa tayari kujumuishwa kwenye kikosi kitakachocheza michuano ya barani Ulaya, kwa ajili ya kuweka usalama wake endapo atasajiliwa na Fc Barcelona.

Cesc Fabregas jana alianza mazoezi sambamba na kikosi kamili cha klabu ya Arsenal, na atasafiri na kikosi hicho hadi nchini Ureno kwa ajili ya mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Benfica utakaochezwa mwishoni mwa juma.

No comments:

Post a Comment