KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 8, 2011

DOGO AMKOSHA CAPELLO.


Siku moja baada ya kuonyesha uwezo uliopelekea Man Utd kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Man city, Tom Cleverley ameongezwa katika kikosi timu ya taifa ya Uingereza ambacho juma hili kitashuka dimbani kupambana na Uholanzi.

Cleverley mwenye umri wa miaka 21, kwa mara ya mwisho alikichezea kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza chini ya umri wa miaka 21, ambacho kilishiriki michuano ya kombe la ulaya mwezi June mwaka huu.

Kuitwa kwake katika timu ya taifa ya wakubwa kunaongeza idadi ya wachezaji wa klabu ya Man utd ambayo sasa inafikia wachezaji watano ambao ni Rio Ferdinand, Michael Carrick, Ashley Young, Wayne Rooney pamoja na Danny Welbeck.

Kocha Fabio Capello ambae jana alikua miongoni mwa mashuhuda wa mchezo wa kuwania ngao ya hisani, alivutiwa na kiwango cha Tom Cleverley, ambacho kilisaidia kupatikana kwa bao la pili la kusawa la Man Utd ambalo lilifungwa na Luis Nani.

Tom Cleverley kwa kipindi kirefu amekua hapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ya mjini Manchester na matokeo yake, meneja Sir Alex Ferguson alilazimika kumtoa kwa mkopo katika vilabu vya Wigan Athletics, Leicester City pamoja na Watford.

No comments:

Post a Comment