KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 12, 2011

Dominic Adiyiah AFUNGUKA BAADA YA KULALAMIKIWA.


Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Dominic Adiyiah amesema alikua sahihi kufanya maamuzi ya kukubali kujiunga na klabu ya ligi daraja la pili nchini Uturuki Karsiyaka FC akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Italia AC Milan.

Dominic Adiyiah amelazimika kulizungumzia suala hilo, baada ya wadau wa soka nchini Ghana kumlaumu kufuatia maamuzi aliyoyachukua ya kukubalia kuichezea klabu ya lifi daraja la pili akitokea kwenye kwenye klabu yenye hadhi kubwa duniani AC Milan.

Amesema anatambua kila mmoja alimshangaa kwa maamuzi hayo lakini kwake anajua amefanya maamuzi yaliyo sahihi kutokana na mazingira ya upatikanaji wa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha AC Milan ambacho kimeshamiri wachezaji wenye uwezo mkubwa.

Hata hivyo amedia kwamba kukubali kwake kujiunga na Karsiyaka FC, kumetokana na mipango ya kutaka kuendeleza uwezo wake kisoka kutokana na umri alio nao huku akiamini ipo siku atarejea katika vilabu vikubwa na kutamba kama ilivyo kwa wachezaji wengine kutoka barani Afrika.

Kabla ya kujiunga na Karsiyaka FC, Dominic Adiyiah mwenye umri wa miaka 21, alipelekwakwa mkopo katika klabu mbili tofauti, ambapo alianzia nchini Italia kunako klabu ya Reggina aliyoitumikia michuzo 13 na kufunga bao moja na kisha alijiunga na Partizan Belgrade ya nchini Serbia.

Dominic Adiyiah, alisajiliw ana Ac Milan mwaka 2010 akitokea klabu ya Fredrik-stad ya nchini Norway na hii ilikua baada ya kung’ara vyema katika fainali za kombe la dunia za vijana chini ya umri wa miaka 20 zilizofanyika nchini Misri mwaka 2009, ambapo kikosi cha Ghana kilitwaa ubingwa baada ya kuifunga timu ya taifa ya Brazil kwa mikwaju ya penati.

No comments:

Post a Comment