KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 11, 2011

Edafe Egbedi AWABEBA WAAFRIKA.


Bao lililofungwa na Edafe Egbedi, katika kipindi cha pili, liliiwezesha timu ya taifa ya vijana ya Nigeria Flying Eagles kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia kwa vijana inayoendelea nchini Colombia.

Kikosi cha Nigeria ambacho tayari kimeshafanikiwa kucheza hatua ya fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa vijana mwaka 1989 na 2005, kimetinga katika hatua ya robo fainali kufautai kisago walichokiporomosha kwa timu ya taifa ya vijana ya Uingereza.

Kocha mkuu wa kikosi cha Nigeria John Obuh amesema haikua kazi rahisi kwa vijana wake kupata ushindi uliowavusha na kuwapelekea katika hatua ya robo fainali kutokana na wapinzani wao kucheza soka la ushindani.

Amesema siri ya mafanikio yaliyopatikana ni kujituma kwa wachezaji wake ambao walifuata maelekezo aliyoyatoa wakati wa mapumziko ambapo timu hizo mbili zilikua bado hazijafungana.

Ushindi huo unaifanya timu ya taifa ya Nigeria kuwa timu pekee kutoka barani Afrika iliyosalia katika fainali hizo za kombe la dunia na katika hatua ya robo fainali itakutana na na timu ya taifa ya Ufaransa.

No comments:

Post a Comment