KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 24, 2011

Emmanuel Adebayor ANUKIA SPURS.


Klabu ya Tottenham Hotspur ipo mbioni kukamilisha dili la kutaka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji toka nchini Togo na klabu ya Manchester City, Emmanuel Adebayor ambae kwa sasa ana mazingira magumu ya kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Roberto Mancini.

Tottenham Hotspur wana matumaini makubwa ya kukamilisha utaratibu huo huku wakikabiliwa na changamoto kubwa ya kumtaka mshambuliaji huyo kukubali kulipwa mashahara wake kwa juma chini ya paund 170,000 ambao amekua akilipwa huko Etihad Stadium.

Meneja wa Spurs Harry Redknapp amesema kwa sasa mazungumzo yanaendelea na dalili za mshambuliaji huyo kukubali kulipwa chini ya mshahara huo zimeshaanza kuonekana hivyo hana wasi wasi na hatua ya kumuona Adebayor akiitumikia klabu hiyo ya kaskazini mwa jiji la London msimu huu.

Hata hivyo amedai kwamba bado kuna changamoto nzito ambayo inaendelea kumkabili kichwani mwake ya kuhakikisha kikosi cha Spurs kunapata uiamara zaidi kama ilivyokua msimu uliopita ambao ulishuhudia wakicheza ligi ya mabingwa barani Ulaya na kufika katika hatua ya robo fainali.

Mwezi januari mwaka huu Emmanuel Adebayor, alipelekwa kwa mkopo katika klabu ya Real Madrid baada ya mambo kumuendea kombo huko Etihad Stadium, na mwishoni mwa msimu aliamini huenda The Galacticos wangemsajili moja kwa moja lakini ndoto hizo ziliingia gizani.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amekua na ugomvi na meneja wa Man city wa kutaka kujumuishwa katika kikosi cha kwanza kama mkataba wake unavyoelekeza, na kila anapohitaji suala hilo likamilishwe hujikuta anaingia katika vita ya maneno na Roberto Mancini.

No comments:

Post a Comment