KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 30, 2011

FA WAUTIA KUFULI UHAMISHO WA Romelu Lukaku.

Mipango ya Chelsea ya kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wao lutoka nchini Ubelgiji, Romelu Lukaku kuelekea Stoke city imegonga mwamba, kufuatia sheria za uhamisho zilizowekwa na chama cha soka nchini Uingereza.

Viongozi wa klabu hizo walikua katika mazungumzo ya kukamilisjha uhamisho wa mkopo wa Romelu Lukaku lakini kizuizi kimeonekana baada ya kuwasilisha jina la mshambuliaji huyo katika ofisi za chama cha soka FA.

Sheria za usajili nchini Uingereza zinaelekeza kwamba, mchezaji yoyote aliesajiliwa katika kipindi hiki, hatoruhusiwa kusajiliwa kwa mkopo katika vilabu vya ndani, zaidi ya kuruhusiwa kuondoka kwa mkopo nje ya nchi hiyo.

Stoke City waliamini huenda wangempata kisahisi mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18 kufuatia uhalisia wa kikosi cha Chelsea ambao haumpi nafasi Lukaku ya kucheza kila juma kama anavyohitaji yeye binafsi.

Uhalisia ndani ya kikosi cha Chelsea, unaonekana kutoa nafasi za kutosha kwa washambuliaji ngulu kama Didier Drogba, Fernando Torres pamoja na Nicolas Anelka.

Hata hivyo mwishoni mwa juma lililopita Romelu Lukaku alipata nafasi ya kuichezea kwa mara ya kwanza Chelsea, akitokea benchi baada ya kuumia kwa mshambuliaji Didier Drogba katika mchezo wa ligi dhidi ya Norwich city waliokubali kibano cha mabao matatu kwa moja.

Romelu Lukaku amesajiliwa na Chelsea katika kipindi hiki, kwa ada ya uhamisho wa paund million 18 akitokea nchini Ubelgiji kwenye klabu ya Anderlecht.

No comments:

Post a Comment