KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 4, 2011

FC BARCELONA NA MATUMAINI YA KUMSAJILI CESC.

Raisi wa mabingwa wa soka nchini Hispania pamoja na barani ulaya kwa ujumla FC Barcelona Sandro Rossell, anadaiwa kumtumia ujumbe mfupi wa simu nahodha na kiungo wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas ambao unamtaka kuwa mtulivu katika kipindi hiki ambacho anahusishwa na uhamisho wa kutaka kurejea nyumbani.

Sandro Rossell, anadaiwa kufanya hivyo kwa kuamini kwamba bado wana nafasi nyingine ya kukamilisha dili la kumsajili Fabregas, kufuatia dili la mwanzo lililotakiwa kukamilishwa mwanzoni mwa juma hili kupigwa chini na viongozi wa Arsenal.

Ujumbe huo mfupi aliotumiwa Cesc Fabregas unadaiwa kusomeka kwamba “usiwe na wasiwasi endelea kuwa mtulivu kwani mazungumzo bado yanaendelea”.

Arsenal waliwapa Fc Barcelona hadi siku ya jumatatu kuhakikisha dili la uhamisho wa mchezaji huyo limekamilishwa, lakini mambo yalikwenda mrama kufuatia mabingwa hao wa soka barani ulaya kushindwa kuwasilisha kiasi cha pesa kinachotakiwa huko Emirates Stadium.

FC Barcelona bado wanandoto za kumsajili Fabregas kwa ada ya uhamisho chini ya paund million 40 ambazo zinatakiwa na Arsenal, na mpaka sasa wameshajinaji kuwa tayari kutoa kiasi cha paund million 33.


Katika hatua nyingine Cesc Fabregas hii leo alitarajiwa kujumuika na wachezaji wengine wa Arsenal katika upigaji wa picha ya pamoja kwa ajili ya msimu wa mwaka 2011-12 ambayo inadhihirisha kuwa mchezaji atakaeichezea klabu hiyo.

Cesc Fabregas pia anatarajia kuanza mazoezi mepesi mwishoni mwa juma hili na huenda akajumuishwa katika kikosi kitakachoanza michezo ya ligi mwishoni mwa juma lijalo ambapo Arsenal watafunga safari kuelekea St James Park kucheza na Newcastle Utd.

No comments:

Post a Comment