KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 23, 2011

FC BARCELONA NA SAKATA LA JOSE MOURINHO.


Makamu wa raisi wa mabingwa wa soka nchini humo FC Barcelona Josep Maria Bartomeu amesema katu hawatojiingiaza katika suala la meneja wa Real Madrid Jose Mourinho ambae juma lililopita alionyesha kitendo cha utovu wa nidhamu wakati wa mchezo wa pili wa kuwania Spanish Super Cup.

Josep Maria Bartomeu, amesema suala la meneja huyo kutoka nchini Ureno linaihusu klabu yake ya Real Madrid ambayo inastahili kumfunda adabu kwa kile alichokionyesha uwanjani.

Amesema litakua jambo la aibu kubwa endapo watajiingiza katika suala la Jose Mourinho, ili hali yupo chini ya uongozi wa klabu iliyoingioa nae mkataba ambao una lengo la kuendeleza mazuri na si mambo mabaya kama ilivyoonekana huko Camp Nou.

Kama itakumbukwa vyema katika mchezo wa pili wa Spanish Super Cup Jose Mourinho, alimsukuma na kumfinya jicho meneja msaidizi wa Fc Barcelona Tito Vilanova, ikiwa ni dakika chache baada ya beki wa pembeni wa Real Madrid Marcelo kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia rafu aliyomchezea Cesc Fabregas.

Wakati huo huo makamu wa raisi wa Fc Barcelona, ametangaza mafanikio ya kuokoa kiasi cha fedha cha Euro million 40, katika usajili wa wachezaji waliowasajili katika kipindi hiki.

Amesema jumla ya kiasi cha pesa ambacho huenda wangekitumia katika usajili wa viungo Cesc Fabregas alietokea Arsenal pamoja na Alexis Sanchez alietokea Udinese ya nchini Italia ni Euro million 110, lakini walijitahidi na kutumia Euro million 70 kwa wachezaji hao.

Amesema Arsenal walimuweka sokoni Fabregas kwa kiasi cha Euro million 60 na Udinese walimueka sokoni Sanchez kwa kiasi cha Euro million 50.

Na taarifa tulizozipata muda mcheze uliopita zinaeleza kwamba:

Shirikisho la soka nchini Hispania limeanza kufanya uchunguzi wa suala la Jose Mourinho kumsukuma na kumfinya jicho meneja msaidizi wa Tito Vilanova katika mchezo wa pili wa kuwani Spanish Super cup.

Uchunguzi huo utategemea sana picha za televishenia mbazo zinaonyesha ni vipi Jose Mourionho alivyohama katika benchi la ufundi la real Madri na kwenda katika benchi la ufundi la Fc Barcelona na kuanzisha hicho kisanga.

Shirikisho la oska nchini Hispania pia limetangaza kuwafungia mchezo mmoja wachezaji walioonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo huo baada ya kutokea kwa zogo lilizosababishwa na adhabu iliyomkuta Marcelo ambae alimchezea rafu mbaya Fabregas.

Wachezaji hao ni Mesut Ozil pamoja na David Villa ambao wanaungana na Marcelo.

No comments:

Post a Comment