KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 4, 2011

FC BARCELONA WAFUNDISHWA SOKA BARANI AMERIKA.


Mabingwa wa soka barani ulaya Fc Barcelona usiku wa kumaki hii leo wamekiona cha mtema kuni kufuatia kisago walichokipokea kutoka kwa washindi wa nane katika ligi ya nchini Mexico Club Deportivo Guadalajara.

FC Barcelona ambao wapo barani Amerika wakifanya maandalizi ya msimu mpya wa ligi, wamepokea kisago cha mabao manne kwa moja ambacho kimewshangaza wenginambao walikua hawaamini kama mabingwa hao wa Hispania wanaudhaifu wa kufungwa idadi hiyo ya mabao.

Mchezo huo uliounguruma nchini Marekani, ulishuhudia FC Barcelona wakianza kupachika bao lao pekee kupitia kwa mshambuliaji David Villa na kisha baada ya hapo walianza kuruhusu kuchezea bakora kutoka kwa wapinzani wao.

No comments:

Post a Comment