KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 25, 2011

Fenerbahce KUWASILISHA RUFAA YAO UEFA.

Klabu bingwa nchini humo Fenerbahce inajipanga kuwasilisha rufaa katika ofisi za shirikisho la soka barani ulaya UEFA ya kupinga maamuzi ya shirikisho hilo, kuwaondoa katika michuano ya ligi ya mabingwa barani humo msimu huu wa mwaka 2011-12.

Fenerbahce wametangaza dhamira hiyo huku ikiwa tayari shirikisho la soka barani Ulaya UEFA likiwa limeshawaidhinisha washindi wa pili wa ligi ya nchini Uturuki msimu uliopita Trabzonspor kuiwakilisha nchi hiyo katika michuano ya ligi ya mabiungwa barani Ulaya.

UEFA wamelazimika kuiondoa Fenerbahce, katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu, kufuatia sakata la upangaji wa matokeo linaloendelea nchini Uturuki ambalo pia lilipelekea raisi wa klabu hiyo, Aziz Yildirim pamoja na zaidi ya wachezaji 30 kutiwa mbaroni na jeshi la polisi.

Fenerbahce, wanadaiwa kupanga matokeo katika baadhi ya michezo ya ligi ya nchini Uturuki msimu uliopita na hatua hiyo ilipelekea kutwaa ubingwa ambao unadaiwa haukuwa halali kwao kufuatia mchezo mchafu walioufanya.

Kuondolewa katika michuano ya ligi ya mambingwa msimu huu, kunaifanya klabu hiyo kukosa sehemu ya fedha walizopanga kuzipata, kutokana na ruzuku inayotolewa na UEFA pamoja na mapato ya mauzo ya tiketi ambayo yangepatikana katika michezo ya barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment