KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 8, 2011

Fernando Gago KURUDI NYUMBANI.


Hatimea kiungo alikosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid Fernando Gago, anakaribi kuihama klabu hiyo na pengine atarejea nyumbani kwao Argentina kujiunga na Boca Juniors.

Wakala wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, Marcelo Lombilla amesema harakati za Gago kuondoka nchini Hispania zinaonyesha matumaini makubwa na kabla ya kumalizika kwa muda wa usajili atakua amefanikisha safari ya kurejea nyumbani.

Marcelo Lombilla amesema mpaka sasa bado ofa ya Boca Junior haijatumwa huko Estadio Stantiago Bernabeu, lakini amekuana na mazungumzo na viongozi wa klabu hiyo ya mjini Buenos Aires ambao wamemuhakikishia kufanya hivyo kabla ya muda haijamalizika.

Fernando Gago, amekua na wakati mgumu wa kupewa nafasi katika kikosi cha kwanza toka alipowasili meneja kutoka nchini Ureno Jose Mourino, hatua ambayo imekua haimpi raha yeye kama mchezaji mwenye kiwango cha hali juu.

Kabla ya kusajiliwa na Real Madrid mwaka 2007, Fernando Gago alikua akiitumikia Boca Junior na akiwa huko kuanzia mwaka 2004 alicheza michezo sabini na kufanikiwa kupachika bao moja.

No comments:

Post a Comment